Mkenya Anayezaa Watoto Mapacha Pekee Adaiwa Amerogwa

Mwanamke mmoja wa nchini Kenya amekimbiwa na mumewe akidaiwa amerogwa na amelazimika kuwalea peke yake watoto wake 12 aliowazaa kufuatia mimba sita za watoto mapacha.
Mama mmoja wa nchini amekimbiwa na mumewe baada ya kuzaa mara sita watoto mapacha hali iliyomfanya mumewe na ndugu zake waamini kuwa si bure bali amerogwa.

Gladys Bulinya alijifungua kwa mara ya sita watoto wawili mapacha mwaka jana lakini ujio huo wa watoto mapacha haukupokelewa vizuri na mumewe ambaye aliamua kukimbia akidai Gladys amerogwa.

Kwa mujibu wa tamaduni za baadhi ya jamii za Kenya, watoto mapacha huonekana ni mkosi kwenye familia na huaminika kuwa huleta bahati mbaya na hutishia maisha ya wazazi .

Gladys alijifungua mapacha wake wa kwanza mwaka 1993 baada ya kupachikwa mimba akiwa sekondari.

Wazazi wake waliwakataa watoto hao na kumlazimisha Gladys awatelekeze hospitalini. Mpenzi wa Gladys alikubali kuwachukua watoto hao na kuanza kuwalea tangu wakati huo hadi leo.

Gladys aliozeshwa kwa mwanaume mwingine mzee kutoka mji mwingine ili kuficha aibu ya familia. Gladys alizaa mara tano na mara zote alikuwa akijifungua watoto wawili mapacha.

Baada ya kujifungua kwa mara ya sita watoto mapacha, mume wake naye aliamua kuingia mitini na kumtelekeza Gladys akiwa na watoto wake 10 aliokuwa akiishi nao.

Gladys mbali ya kukimbiwa na mumewe ametengwa pia na familia yake akionekana kuwa amerogwa. Anaendeleza maisha yake kwa kazi za kubangaiza za kutafuta chakula cha kuwalisha watoto wake.

Miaka na majina ya watoto mapacha wa Gladys:

1993: John na James walizaliwa
1999: Duncan na Dennis walizaliwa
2003: Mercy na Faith walizaliwa
2005: Carren na Ivy walizaliwa
2007: Purpose na Swin walizaliwa
2010: Baraka na Prince walizaliwa

source nifahamishe

 

About fccollection

Am computer administrator........
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a comment