UZINDUZI WA SKULI MPYA YA KISASA BOPWE – PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein, akikata utepe na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe, Alfonso  Lenhardt, kuashiria uzinduzi wa Skuli ya Sekondari ya Bopwe,wilaya ya Wete kaskazini Pemba jana.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt  akiwapongeza wasoma utenzi  Zuhura Khamis na  Samira Bakari, walipohani utenzi wao wakati wa sherehe za uzinduzi wa Skuli Mpya ya kisasa ya Bopwe,wilaya ya wete,Jimbo la Gando jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohammed Shein,akizungumza na wazee na wanafunzi na wananchi wa Jimbo la Gando,wakati wa sherehe za uzinduzi wa Skuli mpya ya kisasa ya Bopwe, Jimbo la Gando, wilaya ya Wete jana, iliyojenga kwa Msaada wa Serikali ya Marekani na Serikali ya mapinduzi Zanzibar.
Mwalimu  Viwe Omar Sharif  akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,na Balozi wa Marekani Nchini  Alfonso Lenhardt, walipotembelea darasa la wanafunzi baada ya ufunguzi rasmi wa Skuli ya Bopwe jimbo la Gando jana.
Advertisements
Posted in Uncategorized | Leave a comment

Dr.Sheni ziarani Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Dk Ali Mohamed Shein,akiwahutubia wananchi wa CCM wa Mikoa miwili ya Pemba,na kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu uliopita,mwaka jana na kuwa Rais wa zanzibar,katika Uwanja wa Bandataka jana

BAADHI ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Dk Maua Daftari alipowasili viwanja vya Bandataka, Chakechake kwa ajili ya kuwashukuru wanaCCM wa visiwa vya Pemba.

MAMA Mwanamwema Shein pamoja na Dk Maua Daftari pia walikuwepo katika mkutano uliofanyika Bandataka.

Katibu Msaidizi Wilaya ya Wete Pemba Zulfa Abdalla,akisoma risala kwa niaba ya mikoa miwili ya Pemba, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa mikoa hiyo,kwa kufanikisha uchaguzi wa huru na salama kwa kuchagua chama cha Mapinduzi na kuongoza katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu liopita,hatimae Dk Ali Mohamed Shein Kuwa Rais wa Zanzibar

 

 

DK SHEIN AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA – GANDO -WETE

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akipewa maelezo na Waziri wa mawasiliano na Miundombinu,Hamad masoud,alipotembelea kituo cha kampuni ya Mecco inayojenga barabara ya Gando-Wete
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi wa kijiji cha gando,wilaya ya Wete alipotembelea maendeleo ya barabara Gando-Wete, inayojengwa na kampuni  ya Mecco
KATAPILA likiwa kazini ujenzi wa barabara ya Gando – Wete
Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa kiji cha gando,wilaya ya Wete alipotembelea maendeleo ya barabara Gando-Wete, inayojengwa na kampuni Mecco
Pichani Daraja la Kicha lililoko katika wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba, likiwa katika hali mbaya, ikiwa limekatika kutokana na magari yenye uzito mkubwa kupita katika daraja hilo
Posted in Uncategorized | Leave a comment

Ajaribu Kujiua Kwa Kukosa Matiti Makubwa

Mrembo wa Brazil ambaye awali alikuwa akishikilia rekodi ya dunia ya kuwa na matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani na baadae matiti hayo kukatwa ili kuokoa maisha yake, amejaribu kujiua kwa mara ya pili akisema kuwa hawezi kuishi bila ya matiti
Mrembo Sheyla Hershey wa nchini Brazil ambaye mwaka jana matiti yake makubwa yalikatwa ili kunusuru maisha yake alipopatwa na maambukizi kwenye matiti yake, amejaribu kujiua kwa mara ya pili. 

Sheyla alifanya operesheni nyingi za kuongeza matiti yake ili kuvunja rekodi ya kuwa na matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani. Alifanikiwa kuvunja rekodi hiyo lakini aliipoteza rekodi hiyo mwaka jana baada ya madaktari kuamua kuyakata matiti yake ili kuyaokoa maisha yake yalipokuwa hatarini kutokana na maambukizi.

Kutokana na kushindwa kuishikilia rekodi ya dunia ya matiti makubwa, mwezi uliopita Sheyla alijaribu kujiua kwa mara ya kwanza akisema kuwa hawezi kuishi bila ya matiti yake makubwa.

“Bila ya matiti yangu makubwa nachukiza na nakuwa sijielewi”, alisema Sheyla ambaye anaishi Texas nchini Marekani.

Sheyla alishawahi kupatiwa matibabu ya kisaikolojia kutokana na lindi la mawazo la kupoteza kitambulisho chake cha mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko wote duniani.

Jumapili wiki iliyopita, Sheyla alijaribu kujiua kwa mara ya pili kwa kumeza kiasi kikubwa cha vidonge.

Sheyla ambaye ana umri wa miaka 31 bado amelazwa hospitali tangu jumapili akiwa kwenye chumba cha watu mahututi.

“Madaktari hawajui ni wakati gani atazinduka, tunamuombea dua aweze kuzinduka”, alisema mumewe.

source nifahamishe

Posted in Uncategorized | Leave a comment

Siri ya Mapenzi ya Michelle Obama

Katika kusherehekea siku ya wapendanao duniani, mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama amewapa wapendanao siri ya mapenzi kuwa ni ‘Si kwa wapenzi kununiana na kuwa siriasi muda wote bali ni kuchekeshana na kupeana matabasamu wakati wote.
Michelle Obama amesema kuwa siri kubwa ya mapenzi ndani ya nyumba ni kuchekeana na mpenzi wako hivyo kudumisha furaha wakati wote.

Michelle Obama amesema kuwa amekuwa akiitumia njia hiyo kuyadumisha mapenzi kati yake na rais Barack Obama na kwa kweli amefanikiwa katika hilo.

Ingawa ndoa yao imekumbwa na misukosuko mingi ya kimaisha na harakati za kisiasa, ndoa hiyo imetimiza miaka 19 sasa.

Bi Obama alisema kuwa siri kubwa ya kudumu kwa mapenzi ndani ya ndoa yao ni kuchekeshana na kupeana matabasamu wakati wote.

Katika kusherehekea siku ya wapendanao Valentine Day, Bi Obama alisema anatarajia mzee Obama atazama mfukoni na kumnunulia zawadi ya mkufu au hereni za dhahabu.

source nifahamishe

 

Posted in Uncategorized | Leave a comment

SECOND WIFE-RAY

NI UNIQUE STORY-WADAU


‘Hakika katika movie ambayo ningependa niangalie hata leo hii ni Second Wife,Hii ni story ya kipekee,Hakika ray umekuja kivingine,Tunasubiri ujumbe mkubwa kutoka katika mzigo huu.Hizi ni baadhi za message ambazo napokea kila siku kutoka kwa mashabiki na Wadau wa movie wakijaribu kuielezea movie ya SECOND WIFE.Mzigo huu umemalizika rasmi kuchukuliwa picha na sasa kilichobaki ni kuhaririwa tuu.Wadau msiwe na haraka mzigo ndio huo unaingia studio

Hizi ni baadhi za scene za mwisho mwisho

Ally Yakuti akiwa katika setting
Nikivalishwa kilemba


Siku ya maakuli ya kuchukua jiko
On set 

setOn
 


On set 

Crew mzigoni

source raythegreatest

Posted in Uncategorized | Leave a comment

MAHAFALI YA NANE CHUO KIKUU ZANZIBAR-2011

Rais wa zanzibar akimpongeza  Leila kati waliofanyaa vizuri katika baishara na fedha

wahitimu wa shahada ya sheria……..

Rais wa zanzibar akimpongeza mtoto wake Asha Ali Mohammed Shein  aliyehitimu shahada ya law na sheria..

Posted in Uncategorized | Leave a comment

UZINDUZI WA TAMASHA LA SAUTI YA BUSARA ZANZIBAR

WANAMICHEZO wa Kikundi cha Michezo cha Watu wenye ulimavu Zanzibar wakishiriki Uzinduxzi huo.
. NAO  wacheza ngoma ya Mbwa kachoka(beni) wakiwa katika maandamano ya uzinduzi wa Tamasha la Busara Zanzibar.

WASANII wa ngoma ya Benbati nao hawako nyuma katika maonesho ya Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar wakiwa katika Uzinduzi.

WANAWAKE  wakiwa  katika Vazi la kucheza Ngoma ya Mwanadenge wakipita mitaani katika uzinduzi wa tamasha la Sauti ya Busara Zanzibar.

WASANII hao na mambo ya asili ya Muafrika  wakionesha  katika uzinduzi wa Tamasha.

MSANII   Mkongwe wa Zanzibar Halikuniki akiwa na Zumari kupiota wote wakiwa katika Uzinduzi huo wakipita barabara ya Malindi kuelekea katika Viwanja vya Ngome Kongwe.
HIVI  ndivyo ilivyo katika uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.
WASANII wakiwa katika maandamano ya Uzinduzi wa Tamasha wakiwa katika mavyazi ya kiasili ya Afrika  wakiwa katika maandamano wakipita katika mitaa ya Michezani.
WATALII wakipata picha ya Kumbukumbu ya Tamasha la Sauti ya Busara kwa Mwaka 2011 ili kuweka kumbukumbu yao walivyotembelea Zanzibar.
WASANII wa Ngoma ya Kiluwa wakiwa katika  maandamano ya  Uzinduzi wa Tamasha la Sauti ya Busara Zanzibar.
WATALII wakiangalia Maandamano ya Tamasha la Busara yakipita barabara ya Forodhani ikiwa ni ufunguzi wa Tamasha hilo.

source jikunbuke

Posted in Uncategorized | Leave a comment